TUMIENI TAALUMA ZENU KUTATUA CHANGAMOTO ZA MASUALA YA CHAKULA NA LISHE KWENYE JAMII.
Na Mwandishi wetu-TFNC Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, amefungua mafunzo elekezi kwa Waajiriwa wapya wa Taasisi, ambapo amewataka kutumia taaluma zao katika kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya chakula na Lishe zinazoikabili jamii. Dkt. Germana amesema mafunzo hayo ya siku tano yamelenga kuwawezesha waajiriwa hao kujua mifumo mbalimbali ya kiutumishi, itakayowasaidia katika kutatua changamoto hizo, na kutekeleza majukumu mbalimbali ambayo Taasisi imekabidhiwa na Serikali kuyatekeleza. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, akitoa maagizo mbalimbali kwa waajiriwa wapya wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kuhusu sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za utumishi wa umma. “Mimi Matarajio yangu kwenu ni makubwa sana, mnisaidie kutatua changamoto za chakula na lishe kwa jamii na ndiyo changamoto ambazo sisi kama Taasisi n