WAAJIRI WAHIMIZWA KUWASAIDIA WANAWEKA KUNYONYESHA WATOTO HUKU WAKIENDELEA NA KAZI.
WAAJIRI
WAHIMIZWA KUWASAIDIA WANAWEKA KUNYONYESHA WATOTO HUKU WAKIENDELEA NA KAZI.
Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amefungua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji maziwa ya Mama kitaifa kwa mwaka 2023, ambapo amewahimiza waajiri katika sekta rasmi na zisizo rasmi na jamii kwa ujumla, kuwasaidia wanawake waweze kunyonyesha watoto wao huku wakiendelea kufanya kazi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Naibu Waziri Dkt. Mollel amesema Maadhimisho ya Mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo “ Saidia Unyonyeshaji: Wezesha Wazazi Kulea Watoto na Kufanya Kazi Zao za Kila Siku” kauli mbiu mbiu ambayo imelenga kuwawezesha wanawake wote wanaofanya kazi katika sekta rasmi na zisizo rasmi kuweza kunyonyesha na kutunza watoto wao ipasavyo.
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wadau wa masuala ya lishe (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi rasmi wa Wiki ya Unyonyeshaji maziwa ya Mama kitaifa kwa mwaka 2023.Aidha
Dkt. Mollel amewakumbusha Viongozi, Wasimamizi,
Watalaam na Watendaji waliopo kuendelea kuelimisha umma kuhusu sheria ya
kulinda haki za Uzazi kwa wanawake, kuimarisha, kuwezesha na kujulisha umma
mifano na hatua za kuigwa zinazochukuliwa
na wadau kwa lengo kuwasaidia wanawake kuendelea kunyonyesha watoto
mahali pa kazi.
Akitoa
salamu za kwa niaba ya Wadau wa Lishe nchini, mwakilisho kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Patric Codjie, amesema Shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kushiriki, kuendeleza na kufanikisha unyonyeshaji kwa
wanawake na litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwawezesha wanawake
walioajiriwa kwenye sekta rasmi na zisizo rasmi wanapata wasaa wa kumpa mtoto
mwanzo bora kupitia unyonyeshaji.
Nchini Tanzania maadhimisho
ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama yalianza kuadhimishwa mwaka 1992, ambapo
huambatana na shughuli
mbalimbali zinazolenga kufikisha taarifa, jumbe na hamasa kwa wananchi kuanzia
ngazi ya Mkoa, Halmashauri na kwenye jamii.
Maoni
Chapisha Maoni