MWENYEKITI BODI YA USIMAMIZI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATUMISHI WA TAASISI

 MATUKIO KATIKA PICHA

Watumishi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wakiwa katika kikao cha pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi Bw.Obey Assery (hayupo pichani) ambapo leo Septemba 14, 2023, anazungumza na Menejimenti na Watumishi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya namna ya kuiwezesha Taasisi kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuleta tija kwa taifa.


Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania  Bw. Obey Assery, akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa Taasisi ( hawapo pichani) ambapo leo amekutana na kuzungumza na watumishi na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Taasisi.


Afisa Rasilimali Watu wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Maurice Nchimbi, akiwasilisha taarifa ya Utumishi kwa  kwa Mwenyekiti  wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi (hayupo pichani), wakati wa kikao chake na Menejimenti na Watumishi wa Taasisi.


Katibu wa Wanawake wa  RAAWU tawi la Taasisi ya Chakula na Lishe Tnzania Bi. Aleswa Swai, akisoma risala ya Wafanyakazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi Bw. Obey Assery (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na Watumishi wa Taasisi kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali  kuhusu Taasisi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tnanzaia Dkt.Germana Leyna, akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 kwa  kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi (hayupo pichani), wakati wa kikao chake na Menejimenti na Watumishi wa Taasisi, kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Taasisi.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.