Machapisho

TFNC YAWANOA WAANDISHI WA HABARI ZA AFYA NCHINI.

Picha
TAAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA, YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI, KUHUSU LISHE SAHIHI KATIKA KUKABILIANA NA COVID- 19. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt: Germana Leyna, akizungumza na Waandishi wa Habari za lishe kutoka vyombo mbalimbali nchini(Hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa semina ya wanahabari hao, juu ya Lishe katika maambukizi ya Virusi vya Corona. Baadhi ya Wandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt: Germana Leyna wakati wa ufunguzi wa Semina kwa wanahabari juu ya Lishe katika maambukizi ya Virusi vya Corona. Afisa lishe mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Medina Wandella, akiwasilisha mada ya matumizi ya matunda na viungo katika kukabiliana na dalili za ugonjwa wa Covid-19, kwa waandishi wa habari za afya, wakati wa semina ya wanahabari hao, iliyohusu Lishe sahihi inayotumika katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vy...

MLONGAZILA YAADHIMISHA MIAKA 200 YA TAALUMA YA UUGUZI

Picha
Mloganzila yaadhimisha miaka 200 ya taaluma ya uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika kumbukizi ya siku ya wauguzi duniani imewapongeza wauguzi kwa kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa lengo ikiwa ni kuonyesha kuwa inatambua na kuthamini mchango wa wauguzi katika kuihudumia jamii. Maadhimisho hayo hufanyika Mei 12, kila mwaka ambapo mwaka huu yana kauli mbiu isemayo “ Wauguzi sauti inayoongoza kwa dunia yenye Afya ”. Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi amewapongeza wauguzi kwa kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma bora za afya huku wakizingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na taaluma hiyo.   “Nawapongeza sana kwa kumbukizi ya miaka 200 ya taaluma ya uuguzi tunatambua na kuthamini mchango wenu kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma huku mkijali utu, taaluma hii ni ya muhimu sana na mnaweza kuwa mmejionea jinsi hospitali inavyoendelea kufadhili masomo ...

UMMY MWALIMU: TUTANDELEA KUTOA AJIRA KWA WAUGUZI NCHINI

Picha
UMMY MWALIMU: TUTANDELEA KUTOA AJIRA KWA WAUGUZI NCHINI Na, WAMJW                         Serikali imesema itaendelea kutoa kipaumbele katika ajira za wauguzi kadri nafasi zitakavyokuwa zikipatikana ili kuboresha huduma za afya nchini. Kauli hiyo imetolewa leo   na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala katika Maadhimisho ya Siku ya Waguzi Duniani   ambayo huadhimishwa tarehe 12 Mei kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wauguzi; Sauti inayoongoza Uuguzi kwa Dunia yenye Afya.” Waziri Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika ajira za wauguzi kwa sababu kuna uhaba wa wauguzi kwenye vituo vya afya licha ya kuwapo zaidi ya wauguzi 30,451 katika vituo vya umma na binafsi nchini. Amesema asilimia 80 ya huduma   za afya ...