MLONGAZILA YAADHIMISHA MIAKA 200 YA TAALUMA YA UUGUZI
Mloganzila
yaadhimisha miaka 200 ya taaluma ya uuguzi
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika
kumbukizi ya siku ya wauguzi duniani imewapongeza wauguzi kwa kutoa huduma bora
za afya kwa wagonjwa lengo ikiwa ni kuonyesha kuwa inatambua na kuthamini mchango
wa wauguzi katika kuihudumia jamii.
Maadhimisho hayo hufanyika Mei 12, kila mwaka ambapo
mwaka huu yana kauli mbiu isemayo “Wauguzi sauti inayoongoza kwa dunia yenye
Afya”.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Kaimu Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth
Magandi amewapongeza wauguzi kwa kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma bora za
afya huku wakizingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na taaluma hiyo.
“Nawapongeza
sana kwa kumbukizi ya miaka 200 ya taaluma ya uuguzi tunatambua na kuthamini
mchango wenu kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma huku mkijali utu, taaluma
hii ni ya muhimu sana na mnaweza kuwa mmejionea jinsi hospitali inavyoendelea
kufadhili masomo kwa wauguzi mbalimbali wanaojiendeleza ili kuboresha utoaji
huduma katika hospitali yetu” amesema Dkt. Magandi.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi akiwapongeza wauguzi wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani |
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi
wa MNH-Mloganzila, Sr. Redemptha Matindi amewaeleza wauguzi kuwa taaluma ya
uuguzi ni taaluma inayohitaji upendo, utu, heshima, kujali na kujitoa ili
kuwapatia wagonjwa huduma stahiki bila kujali uwezo au uofauti wa kipato.
Katika kuadhimisha siku hii wauguzi katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili-Mloganzila walikata keki na kuwasha mishumaa ikiwa ni alama
ya kuwakumbusha kuendelea kutoa huduma kwa upendo, ukarimu, uvumilivu na kujali
utu.
Wauguzi wakiwa wamewasha mishamaa ishara ya upendo, uvumilivu, heshima, ukarimu na kujitoa katika taaluma hiyo. |
Maoni
Chapisha Maoni