TFNC YAHIMIZA WANAOTOA USHAURI WA LISHE MITANDAONI KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZENYE MAMLAKA
Amesema kaulimbiu ya taasisi hiyo katika tamasha hilo ni “Chakula Chetu, Utamaduni Wetu, Afya Yetu,” akisisitiza wananchi kula mlo kamili unaojumuisha vyakula kutoka katika makundi sita ili kupata virutubishi muhimu kwa afya.
Ngilisho amesema elimu hiyo inaambatana na umuhimu wa kuzingatia usafi wa mazingira, maji na chakula, kuepuka matumizi ya vileo, sigara na tumbaku, pamoja na kufanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kila siku.
Kadhalika ameeleza kuwa maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe huchunguza sampuli za vyakula na binadamu ili kubaini virutubishi na upungufu wa vitamini au madini, huku matokeo yakitumika kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali kuhusu hatua za kukabiliana na changamoto za lishe.
Maoni
Chapisha Maoni