TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

 

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI 2020.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto) akikabidhi zawadi ya mshindi wa jumla wa maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani kwa mwaka wa  2020 yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe kwa Bi Adeline Munuo kutoka  Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, mara baada ya Taasisi hiyo kuibuka mshindi wa Jumla katika maonesho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Lunyanyo mkoani humo.

Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Adeline Munuo, akiwa pamoja na wafanyakazi wengine wa Taasisi hiyo, wakishangilia mara baada ya kupokea tuzo ya Ushindi wa jumla ya  Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya chakula Duniani kwa mwaka wa 2020 kutoka kwa Waziri wa kilimo Japhet Hasunga (Mwenye suti nyeusi), ambaye aliitimisha maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Njombe.


Afisa Lishe Mtafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Elizabeth Lyimo, akifurahi ushindi wa Taasisi hiyo, mara baaba ya kuibuka mshindi wa jumla katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani kwa mwaka wa 2020 ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Njombe


Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.