TFNC-KUENDELEA KUSHIRIKIA NA WADAU UTEKELEZAJI AFUA MBALIMBALI ZA LISHE
Na. Mwandishi Wetu –Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Chakula na Lishe Tanzani Dkt. Germana Leyna, amesema Taasisi ya Chakula na
Lishe itaendelea kushirikiana na wadau katika masuala mbalimbali yanayohusiana na lishe, ili kuweza kutekeleza
afua za kilishe kwa pamoja.
Hayo yamebaninishwa Jijijin Dar
es Salaam, wakati wa kikao kati ya Mkurungezi Mtendaji wa wa Taasisi ya Chakula
na Lishe Dkt. Germana Leyna na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
SANKU Bw. Felix Brooks-Church, kilichofanyika katika Ofisi za Shirika hilo zilizopo
Masaki.
Katika kikao hicho, aidha Dkt.
Germana alipata wasaa wa kufahamu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na
shirika hilo katika kuimarisha suala la Uongezaji wa virutubisho vya madini na
Vitamini katika vyakula, kupitia teknolojia ya mashine zinazofungwa kwenye
Mashine za kusanga unga wa Mahindi.
Mkurungezi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la SANKU ( hayupo pichani) wakati alipotembea ofisi za Shirika hilo, kujifunza na kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa afua ya urutubishaji unaofanyika katika kwa Viwanda vidogo na vya kati vinavyozalisha bidhaa za unga wa Mahindi
“Serikali ipo pamoja nanyi na
sisi kama Taasisi tupo tayari kuendelea kushirikiana na kuwapa ushauri wa
kitaalamu ili kwa pamoja tuweze kushirikiana katika kuimarisha lishe za
Watanzania” alisema Dkt. Germana.
Katika Hatua nyingine Dkt. Germana amewapongeza SANKU kwa jitihada zao wanazochukua katika kusambaza teknolojia yao inayotumika katika urutubishaji wa bidhaa za unga wa mahindi, ambapo amesema zimesaidia kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia unga wenye virutubishi vya madini na Vitamini na kusaidia kupunguza idadi ya wananchi wenye upungufu wa virutubishi hivyo muhimu mwilini.
Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la SANKU Felix
Brooks- Church akitoa maelezo kwa Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Chakula na
Lishe Tanzania ( hayupo pichani) namna wanavyotekeleza majukumu yao katika
kuwawezesha wasindikaji wadogo na wa kati wa unga wa mahindi kupata
virutubishi, vifungashio na vinyunyizi (Dosifiers) kwa ajili ya kuongeza
virutubishi kwenye unga wa mahindi unaozalishwa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna alitembelea Ofisi za shirika la
SANKU na kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa afua za urutubishaji wa unga wa
mahindi unaotekelezwa na viwanda hivyo, ambavyo vimekuwa vikiwezeshwa teknolojia
rafiki kutoka kwa Shirika la SANKU.
MWISHO:
Maoni
Chapisha Maoni