GAIN KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUONGEZA VIRUTUBISHI KWENYE CHAKULA

Na.Mwandishi wetu- Dar es Salaam.

Shirika la Global Alliance For Improved Nutrition (GAIN) limesisitiza  litaendelea kushirikiana na Serikali hususani kupitia Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, kuendelea kuelimisha  umma  juu ya umuhimu wa kutumia vyakula vilivyoongezwa virutubishi ikiwemo unga wa Mahindi, Ngano, Mafuta ya Kupikia pamoja na Chumvi. 

Hayo yamebainishwa na  Msimamizi wa programu ya urutubishaji kutoka shirika la GAIN Dkt. Archard Ngemela wakati akizungumza na  Maafisa Utafiti wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania, wakati wa Semina ya majadiliano kuhusu umuhimu wa urutubishaji wa vyakula kwa ngazi ya Viwanda iliyofanyika hivi karibuni.

Dkt.Ngemela amesema shirika la GAIN limejikita zaidi kuhakikisha linasaidia serikali kwenye upatikanaji wa Virutubishi, upatikanaji wa mashine za kuchanganya virutubishi  hivyo kwenye unga pamoja na kuwajengea uwezi watendaji wa ngazi za Mikoa na Halmashauri katika usimamizi wa ubora wa urutubishaji.

“Kwa sasa GAIN tumesaidia Serikali kununua mashine 50 ambazo zimetengezwa hapa hapa nchini na SIDO kwa gharama ya Milion 60, na tutazigawa kwa vyama vya wazalishaji mahindi katika mikoa ya Kagera, Mara, Iringa, Kilimanjaro na Manyara ikiwa ni jitihada za kuisaidia Serikali kufikia malengo ya kununua mashine 300 ili kuboresha huduma ya urutubishaji vyakula nchini.”alisema Dkt.Ngemela

Aidha Dkt.Ngemela amesema kwa upande wa kuwajengea uwezo wataalamu, amesema wameendelea kushrikiana na serikali kwani hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwajengea uwezo wataalamu 120 wakiwemo maafisa lishe, Wataalamu wa maabara na maafisa ya Lishe ambao ndiyo wanasimamia ubora wa vyakula vilivyorutubishwa.

“Tayari tumewafikia Maafisa lishe, Maafisa afya na wataalamu wa Maabara katika mikoa ya Kilimanjaro, Mara, Kagera,na Iringa na kuwajengea uwezi kuhusu namna ya kufanya uchambuzi wa kimaabara ili kubaini viwango vya madini na vitamin kwenye vyakula vilivyofanyiwa urutubishaji.” Alisema Dkt. Ngemela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, amewapongeza GAIN kwa jitihada wanachukua katika kufanikisha  urutubishaji wa vyakula vilivyoognezwa virutubishi, na Serikali kupitia Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania wako tayari kushirikiana na Shirika hilo katika  kuelimisha  umma  juu ya umuhimu wa kutumia vyakula hivyo ili kusaidia Watanzania kuepukana na matatizo ya upungufu wa madini na Vitamini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.