WENYE KIFUA KIKUU NA VVU KUPATA ELIMU YA LISHE KIGANJANI

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamezindua Programu ya Simu inayohusu Masuala ya Lishe kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI pamoja na kifua kikuu ili kusaidia kukabiliana na magonjwa nyemelezi na kuimarisha hali zao za lishe.

Akizundua Programu hiyo Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema programu hiyo itaongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na magonjwa hayo na ikiwezekana kuyatokomeza kabisa. 

Programu hiyo kwa sasa itapatikana kwenye simu zenye mfumo wa Android na baadae kwenye simu zenye mfumo wa IOS na ambayo itamuwezesha mgonjwa wa kifua kikuu na mtu anayeishi na ugonjwa wa UKIMWI kumwezesha kupata erlimu yam lo kamili kupitia video na majarida mbalimbali pamoja kujfanyia tathmini ya hali yake la lishe.

"Lishe hii ni moja ya mikakati ya kuwajengea wananchi uelewa kuhusu masuala ya lishe bora na kuchochea mfumo bora wa lishe,kupitia programu hii naamini Itasaidia kutoa elimu na ujuzi namna ya kuandaa milo na kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo husika,

 


Hii Itasaidia kufikia malengo ya wizara ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza,"amesema Prof Nagu.

Ili kufanikisha malengo ya serikali, Profesa Nagu ameitaka TFNC kuihakikisha kupitia Programu hiyo inawafikia watu wengi zaidi wakiwamo wenye magonjwa ya Kisukari na Saratani

Makundi mengine aliyoagiza Profesa Nagu  yafikiwe ni  watoto wadogo, wachanga,vijana balehe; wajawazito na wanawake wanaonyonyesha pamoja na; makundi mengine ili kuongeza chachu ya mabadiliko chanya katika ulaji unaofaa na mitindo bora wa maisha.

Pia ameiagiza taasisi hiyo kubuni njia za kuwafikia wanaume ili kuleta uelewa wa pamoja katika familia kwa lengo la kukinga badala ya kutibu.

 


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzaniaa, Dkt.  Germana Leyna amesema mwaka 2020 walifanya tathmini  katika mkoa wa Geita na Singida  kuangalia hali za lishe na uelewa wa huduma za afya kwa watu wenye VVU na kubaini kundi hilo lina uelewa mdogo.

Amesema katika mahojiano yao ya ana kwa ana na watu wenye VVU takribani 20 na kubaini 18 hawana uelewa wa masuala ya lishe.

"Walikuwa hawana taarifa kamili japo namba ya idadi ni ndogo lakini kwetu ilikuwa  inaonekana  elimu hii haijawafikia watu kwenye vituo vya afya japo  watoa huduma wapo,

 Tunajua kuna changamoto labda wanazidiwa na kazi au muda sio rafiki lakini tuliona kwamba bado wanahitaji elimu, kwa hiyo ilikuwa elimu hiyo tuiotoeeje ili kufikia watu wengi zaidi, ndipo wazo la kutumia App ya kiganjani ilipokuja,"amesema Dkt. Germana Leyna.

 


Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Bi.Sarah Gordon-Gibson amesema wataendelea kuwekeza kwenye lishe na kuendelea kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Taasisi ya Chakula na Lishe katika kukabiliana na afua mbalimbali za lishe ikiwemo zile ambazo zinaelekezwa kwenye Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bw.Obey Assey amesema haya ni mapinduzi makubwa ambayo yamefanyika kwenye Masuala la lishe na kupitia programu hiyo itaweza kuwafikia watu wengi zaidi huku kuitaka Menejimenti ya Taasisi kuhakikisha wanaisimamia programu hiyo na hata iweze kutumika kuwafikia makundi mengine.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.