WATAALAMU PROGRAMU YA USI WAZURU MKURANGA

 Mwanasayansi na mtaalamu Mbobezi wa program ya Chumvi (USI) kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Dkt. Rizwan Yusuf pamoja na wataalamu wengine kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wamefanya ziara katika halmshauri ya Mkuranga  na kukutana na wadau wa chumvi ili kujadili utekelezaji wa program ya kuzuia upungufu wa madini joto.

Katika ziara hiyo watalaamu hao, pia wamejadiliana juu ya uzalishaji na uchakataji wa Chumvi yenye madini joto na namna ya kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli za programu hiyo katika halmashauri ya Mkuranga.

Watalaamu hao wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dk. Germana Leyna wamefanikiwa kutembelea mashamba ya wazalishaji Chumvi wa Halmashauri hiyo, na kujionea namna wazalishaji chumvi hao namna wanavyochanganya chumvi na madini joto, kabla ya kuyaingiza sokoni.

Pia timu hiyo ya Wataalamu imetembelea kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkhanth Salt Limited kilichopo Mkuranga na kujionea namna shughuli za uzalishaji wa Chumvi yenye madini joto zinazofanyika kiwandani hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna (mwenye mtandio) akiangalia mashine ya kuchanganya chumvi na madini joto namna inavyofanya kazi, mara baada ya kutembelea shamba la wazalishaji chumvi wa kikundi cha Kiumbo Salt katika Halmashauri ya Mkuranga, ikiwa ni zara ya  kukutana na wadau wa chumvi ili kujadili utekelezaji wa program ya kuzuia upungufu wa madini joto.

Mwenyekiti wa kikundi cha wazalishaji chumvi cha Kiumbo kilichopo halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani, akielezea namna wanavyoshirikiana na wataalamu wa programu ya Chumvi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, kuhakikisha chumvi wanayozalishwa inachanganywa na madini joto.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.