WANANCHI KARAGWE NA KILOLO WAPATIWA ELIMU YA LISHE BORA

Jumla ya wananchi 159 wa vijiji vya Omurusimbi wilayani Karagwe na Igunga wilayani Kilolo wamepatiwa elimu ya Lishe ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya na lishe ya kijiji.


Mafunzo hao yametolewa katika vijiji hivyo vya mikoa ya Kagera na Iringa ikiwa na muendelezo wa maadhimisho hayo kila baada ya miezi mitatu ambapo huduma mbalimbali za afya na lishe hutolewa kwa wananchi

Elimu hiyo imejumuisha namna ya kuandaa na kula mlo kamili kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika vijiji vyao huku ikilenga kupunguza tatizo la utapiamlo ikiwemo udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.


Vile vile wananchi hao wamepatiwa elimu ya ulaji wa mlo kamili ili kuepuka utapiamlo hususan udumavu kwa watoto.


Lishe bora ni muhimu kwa afya ya binadamu na hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya Moyo,Kisukari,Shinikizo la damu,kuongeza uwezo wa mwili kufanya kazi na kuepuka tatizo la utapiamlo hasa wa mwili na akili kwa watoto chini ya miaka mitano



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.