TUTAYAFIKIA MAKUNDI YOTE KWENYE UTOAJI WA ELIMU YA LISHE

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Lishe na Mafunzo wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Esther Nkuba, amesema Taasisi itaendelea kutoa elimu ya masuala ya chakula na lishe kwa Watanzania, na kuhakikishia kila mmoja anafikiwa na elimu yakiwemo makundi ya watu wenye mahitaji maalumu.

Dkt. Nkuba amebainisha hayo Machi 10, 2023 Jijinmi Dodoma wakati ufunguzi wa kikao kazi cha kupitia nyenzo rafiki kwa watu wasioona, ambayo itawawezesha kupata taarifa mbalimbali sahihi za masuala ya Chakula na Lishe.


Imeleezwa kuwa nyenzo hizo zimeandaliwa kwa, mfumo wa nukta nundu pamoja na sauti kwa ajili ya kusikilizwa kwa wale wasioweza kusoma maandishi ya nukta nundu.
Dkt. Nkuba amebainisha kuwa kabla ya kuzinduliwa rasmi kuanza kutumika kwa nyenzo hizo ambayo uandaaji wake umefadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP),wadau wa lishe wamekutana na kuzijadili kabla ya kupitishwa kutumika rasmi.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu Wasioona Tanzania Bwa. Omary Itambu, amesema ujio wa nyenzo hizo utakuwa msaada kwao, kwani jamii ya watu wasioona, kwa muda mrefu ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa za lishe na afya ambazo ni muhimu kwao.


Bwa.Itambu amesema kukamilika kwa nyenzo hizo kutasaidia jamii ya watu wasioona kunufaika na jumbe za lishe hususani lishe ya wanawake wajawazito, na mama anayenyonyesha, ulishaji wa watoto wadogo na wachanga, ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha pamoja na lishe kwa watu wanaoishi na VVU, ambazo zote zinapatikana katika nyenzo hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.