TFNC NA WFP YAWAFIKIA WATU WASIOONA KWENYE UTOAJI ELIMU YA LISHE.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kupitia Ufadhili wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) imewafikia watu wasioona, mara baada ya kuzindua nyenzo zenye ujumbe wa lishe kwa kundi hilo, ambazo zimeandaliwa katika maandishi ya nukta nundu na nyingine kwenye mfumo wa sauti.

Hafla fupi ya uzinduzi huo imefanyika Machi 21, 2023, katika Ofisi za Taasisi ya Chakula jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa lishe akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gordon-Gibson.

Akizundua kitabu cha ujumbe huo wa lishe kwa jamii ya watu wasioona, kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji  wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dkt. Esther Nkuba ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya Lishe na Mafunzo, amesema kitabu hicho kinalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii ya watu wasioona kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya watoto na afya ya watu wa jamii hiyo kwa ujumla.


Dkt.Nkuba amesema Taasisi imeyafikia makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, watoto wadogo na wachanga, vijana balehe, na wazee, huku kundi la wasioona likisahulika, hivyo ujio wa nyenzo hii utawasaidia nao kuweza kufikiwa na elimu ya lishe mabayo Taasisi imekuwa ikiitoa.

“Ni matarajio yetu


kuwa jamii ya watu wasioona watanufaika na elimu pamoja na taarifa sahihi za lishe ambazo zitawasaidia kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa lishe kwa afya zao na hivyo kuchochea mabadiliko ya tabia kuhusu kufuata taratibu sahihi.”alisema Dkt.Nkuba


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.