USAID, BILL AND MERINDA GATES FOUNDATION NA HAVARD UNIVERSITY WAZURU TFNC.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania leo Februari 24,2023 imetembelewa na Maafisa kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation pamoja na Chuo Kikuu cha Havard ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kukabiliana na Matatizo mbalimbali ya Kilishe nchini.

Maafisa hao wamefika katika maabara za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania zilizopo Mikocheni na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi Bw.Obey Assey na kujionea shughuli zinazofanywa na Maabara hiyo ikiwemo za upimaji wa virutubishi mbalimbali katika Vyakula.


Mwenyekiti wa Bodi  ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bw.Obey Assey (kushoto) akiwaongoza wageni kutoka USAID, Bill and Merinda Gates Foundation na Chuo Kikuu cha Havard waliotembelea Maabara ya Taasisi hiyo, ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika  maabara ya Chakula ya Taasisi hiyo iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Msimamizi wa Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Tedson Lukindo (Shati la Mistari) akitoa maelezo juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Maabara hiyo kwa Maafisa kutoka USAID, Bill and Merinda Gates Foundation na Chuo Kikuu cha Havard, waliofika kuona namna maabara hiyo inayofanya shughuli zake za upimaji wa virutubishi mbalimbali katika Vyakula.


Msimamizi wa Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Tedson Lukindo, (Shati la Mistari) akitoa maelezo namna shughuli za uhifadhi na upimaji wa sampuli zinavyofanyika katika Maabara hiyo kwa Maafisa kutoka USAID, Bill and Merinda Gates Foundation na Chuo Kikuu cha Havard, waliofika kuona utendaji kazi wa maabara hiyo kwenye upimaji a virutubishi mbalimbali katika Vyakula.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.