WIZARA YA AFYA YAKABIDHI VIFAA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19 KWA MIKOA 17
WIZARA YA AFYA YAKABIDHI VIFAA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19 KWA MIKOA 17
Na, Jackson Monela -Dodoma
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhi vifaa vya kujikinga na UVIKO-19 kwa Mikoa 12 ya Tanzania Bara na 5 ya Zanzibar vilivyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kupitia shirika la Kimataifa la Nutrition International (NI) ikiwa ni kuwakinga watoa huduma ya afya hususani katika zoezi la Utoaji wa Matone ya Vitamini A nchini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa wawakilishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mganga Mkuu wa Serikali Dkt Aifillo Sichalwe amesema vifaa hivyo vitaenda kuwasaidia watoa huduma za afya walio mstari wa mbele katika kutoa huduma za afya nchini bila kuwasahau watoa huduma za afya ngazi ya jamii (CHW)
Dkt Sichalwe amesema kutokana na changamoto ya UVIKO-19 Serikali inaendelea kuwapatia vifaa vya kujikinga na maambukiz ya UVIKO-19 watoa huduma waliopo katika vituo vya afya ili kuwawezesha kuendelea kutoa huduma za afya kwa ufanisi ikiwemo Kampeni ya utoaji wa Matone ya Vitamini A inayofahimika kama Huduma ya Mwezi wa Afya na Lishe ya Mtoto.
Dkt. Masumo amesema vifaa hivi
vitawasaidia watoa huduma ya afya waliopo mstari wa mbele katika kutoa huduma
za afya ikiwemo Huduma ya mwezi wa Afya na Lishe ya Mtoto kwani malengo
yaliyopo ni kuhakikisha ifikapo Mwaka 2025 watoto wote nchini wafikiwe na huduma
ya matone ya Vitamini A kupitia vituo vya afya vilivyopo nchini.
Nae Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Nutrition International (NI) Dkt Daniel Nyagawa amesema wamechukua uamuzi wa kutoa vifaa kwa Serikali ikiwa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazochukuliwa katika kupambana na UVIKO-19 na wataendelea kushirikiana na katika afua nyingine ikiwemo zile za Kilishe ambazo shirika hilo limekuwa likizitekeleza hapa nchini.
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.
Aifillo Sichalwe akikabidhi boksi la Kitakasa Mkono kwa Naibu katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mohamed Abdulla kwa ajili ya Mikoa 5 ya
Zanzibar ikiwa ni ikiwa ni ishara ya
kupokea vifaa vya kuwakinga na UVIKO-19 watoa huduma za afya wakati wa huduma
za Mwezi wa afya na Lishe ya Watoto.
Jumla ya Katoni 6000 za Barakoa (Mask) na Vitakasa Mikono (Sanitizer) lita 6000 vyenye gharama ya Milioni 57 vimetolewa na vitasambazwa katika mikoa 17 ikiwemo 12 ya Tanzania bara na 5 ya Tanzania visiwani.
MWISHO:
Maoni
Chapisha Maoni