ULAJI ASALI NI LISHE, TIBA KWA MAGONJWA HAYA.

Tangu enzi asali imekuwa miongoni mwa bidhaa muhimu ambazo zilitumika kama chakula na kutengeneza dawa.

Asali imekuwa ikitumika kutibu maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na wingi wa viinilishe vingi na vya aina tofauti ambavyo vina faida ya kilishe na tiba.

Asali imekuwa ikitumika kutibu maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na wingi wa viinilishe vingi na vya aina tofauti ambavyo vina faida ya kilishe na tiba.

Miongoni mwa faida za asali ni pamoja na kuzuia upungufu wa damu, kutibu ugonjwa wa mfumo wa hewa na kutibu baadhi ya magonjwa ya mfumo wa chakula.

Mtaalu wa Lishe Kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Medina Wandella anasema wanga uliopo kwenye asali humeng’enywa kwa urahisi na hivyo kusaidia kuwapatia watu nishati lishe (nguvu) wenye matatizo ya kumeng’enya chakula.

“Uwepo wa madini ya iron, copper na manganese husaidia kwenye kutengeneza chembechembe za damu mwili na hivyo kuzuia upungufu wa damu,” Anasema Wandella

Wandella anasema faida nyingine ni kutibu magonjwa ya mfumo wa hewa pamoja na kikohozi kikavu au kinachokereketa, kuzuia vijidudu (anti-microbial), anti- inflammatory, anti-oxidant pamoja na  kutibu vidonda, hasa vinavyotokana na kuungua.

Vilevile asali inaweza kutumika kama tiba ya magonjwa ya mengine ya ngozi yanayosababishwa na bakteria na fangasi. Mtaalamu huyo anasema asali pia hutibu baadhi ya magonjwa ya mfumo wa chakula kama kuhara.

“Asali hudhibiti uwiano mzuri wa lehemu mbaya na nzuri katika damu na ia ni dawa ya usingizi kwa watu wenye matatizo ya kupata usingizi,” anafafanua Wandella

 

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.