MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria imetoa matokeo ya utafiti wa hali ya lishe ya wanafunzi wa Shule za Msingi uliofanyika mwaka 2021 na kuhusisha mikoa 26 ya Tanzania bara. Utafiti huo ulihusisha shule za umma 650 na wanafunzi 64,465 ulilenga kutathimi kiwango cha Maambukizi ya Malaria na Utapiamlo miongoni wa wanafunzi, ambapo katika viashiria vya lishe, utafiti huo umebaini wanafunzi waliopo katika shule za msingi bado wana changamoto nyingi za kilishe zinazowakabili. Akiwasilisha taarifa za utafiti huo kwa wadau mbalimbali wa lishe kutoka Idara za Serikali, Mashirika ya Kimataifa, wadau wa maendeleo, asasi za kiraia na wadau wengine, Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Geofrey Mchau, amesema wameweza kubaini wanafunzi wengi bado wana lishe duni, uzito uliopungua, uzito uliokithiri na upungufu wa damu kwa kiwango kikubwa. Dkt. Mchau amesema utafiti huo umebaini pia mazingira mengi yanayozun...
Maoni
Chapisha Maoni