JUKWAAA LA PAMOJA LA TAARIFA NA TAKWIMU ZA LISHE NCHINI SASA LAZINDULIWA RASMI.
JUKWAAA LA PAMOJA LA TAARIFA NA TAKWIMU ZA LISHE NCHINI SASA LAZINDULIWA RASMI.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akibofya kitufe
katika Kompyuta mpakato Kuashiria uzinduzi rasmi wa Jukwaa la Pamoja la taarifa
na takwimu za Lishe Nchini, Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma Disemba 17, 2020
katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, aliyesimama kushoto kushuhudia uzinduzi
huo ni Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi na kulia
kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt Germana
Leyna.
Mtaalamu wa Mifumo kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es salaam, Idara ya Sayansi ya Uandishi wa Kompyuta Henry Kalisti (Mwenye
Shati rangi ya Bluu) akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu)
Bi. Dorothy Mwaluko namna mfumo wa jukwaa la pamoja la taarifa na takwimu za
lishe nchini namna unavyofanya kazi, mara baada ya kuzinduliwa na katibu mkuu
huyo jijini Dodoma Disemba 17, 2020 katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akimwelezea katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi Dorothy Mwaluko, namna takwimu na taarifa mbalimbali zitakazoingizwa katika jukwaa la pamoja la taarifa na takwimu za Lishe, zitakavyoweza kutumiwa na wadau wa lishe, ambao watahitaji kupatiwa kwa ajili ya matumizi yao.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na watendaji wa Serikali ambao wanatakiwa kusimamia jukwaa la pamoja la taarifa na takwimu za lishe nchini (hawapo pichani) namna ambavyo wanaweze kuendesha jukwaa hilo, ambapo amewataka kuwa makini na matumizi ya takwimu hizo zitakazoingizwa kwenye mfumo
Maoni
Chapisha Maoni