TFNC YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe kutoka Taasisi ya Chakula
na Lishe Tanzania Dkt: Elifatio Towo akitoa maelezo kwa naibu waziri wa Kilimo
Omary Mghumba namna Taasisi hiyo inavyoshiriki katika uelimishaji na utafiti wa
masuala ya Chakula na lishe, mara baada ya Naibu waziri kutembelea banda la Maonyesho
la Taasisi ya Chakula na Lishe mara baada ya kuzindua Maadhimisho ya Siku ya
Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Njombe.
Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi
ya Chakula na Lishe Tanzania Bi Adeline Munuo akitoa elimu ya Masuala ya
Chakula na Lishe kwa kutumia piramidi ya makundi matano ya chakula kwa baadhi
ya wakazi wa Njombe, ambao wamepata fursa ya kutembelea banda la Maonyesho la
Taasisi hiyo, katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani ambayo yanafanyika kitafia mkoani Njombe na
Kilele chake kinatarajiwa kuwa Oktoba 16.
Maoni
Chapisha Maoni