WAZIRI UMMY MWALIMU, AZINDUA RASMI MAADHMISHO YA WIKI LA UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA KWA MWAKA 2020.
WAZIRI UMMY MWALIMU,
AZINDUA RASMI MAADHMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA KWA MWAKA 2020.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akikikata utepe kwenye kitini
cha Lishe ya Wanawake, Watoto na Vijana Balehe kwa ajili ya Vyombo vya Habari, kuashiria kuanza
kutumika rasmi kwa kitini hicho, zoezi ambalo limeenda sambamba na uzinduzi wa Maadhimisho
ya Wiki la Unyonyeshaji maziwa ya Duniani,
ambayo kwa mwaka huu kitaifa yamefanyika wilayani Muheza mkoani Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akimkabidhi Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Tanga Burhan
Yakubu kitini cha Lishe ya wanawake, Watoto na Vijana Balehe kwa ajili ya
Vyombo vya Habari, kuashiria kuanza kutumika rasmi kwa kitini hicho, wakati wa
Uzinduzi wa Wiki la Unyonyonyeshaji maziwa ya Mama Duniani, ambayo kwa hapa
nchini yamefanyika wilayani Muheza mkoani Tanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt: Germana Leyna akitoa taarifa ya hali ya Unyonyeshaji maziwa ya Mama nchini, wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya wiki la unyonyeshaji, ambayo kwa mwaka huu kitaifa yamefanyika Wilayani Muheza mkoani Tanga katika Viwanja vya Jitegemee na kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, yakibeba Kauli mbiu isemayo “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha Watoto kwa afya bora na Ulinzi wa mazingira”.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa maadhimisho
ya Wiki la Unyonyeshaji Maziwa ya mama Duniani (hawapo Pichani) ambayo kwa mwaka
huu uzinduzi huo umefanyika wilayani
Muheza mkoani Tanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akifurahi kwa kucheza mziki na akina
mama waliojitokeza kushiriki kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki la
Unyonyeshaji Maziwa ya mama Duniani, ambayo kwa mwaka huu yamebeba Kauli mbiu isemayo
“Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha Watoto kwa afya bora na Ulinzi wa mazingira” ambapo
uzinduzi huo umefanyika wilayani Muheza mkoani Tanga.
Cicilia Mdugu mkazi wa Muheza
mkoani Tanga, akitoa ushuhuda kwa wananchi waliojitokeza kushiriki kwenye
uzinduzi wa maadhimisho ya wiki la unyonyeshaji maziwa mama Duniani, namna
alivyoweza kumyonyesha mwanae kwa kipindi chote cha miezi sita bila kumpa chakula
na kinywaji chochote.
Maoni
Chapisha Maoni