Ijumaa, 7 Agosti 2020

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA RASMI SIKU YA LISHE, SASA KUADHMISHWA KILA MWAKA KUANZIA NGAZI YA WILAYA HADI TAIFA.

 WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA RASMI SIKU YA LISHE, SASA KUADHIMISHWA KILA MWAKA KUANZIA NGAZI YA WILAYA HADI TAIFA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akikata utepe kwenye  Piramidi ya Lishe, ambayo imebebea mfano wa Vyakula kutoka kwenye makundi matano ya Chakula, kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa  Siku ya Lishe, huku Naibu katibu mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt Doroth Gwajima (mwenye skafu) akishuhudua Uzinduzihuo  ambao umefanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (Kulia), na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Doroth Gwajima (Kushoto) wakipokea maelezo ya vyakula vilivyopo kwenye Piramidi ya Lishe,kutoka kwa Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi Rose Msaki, mara baada ya kuzindua rasmi siku ya Lishe iliyofanyika  kitaifa Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akizungumza na Wananchi wa jiji la Dodoma na Wadau wa Lishe, (Hawapo Pichani) wakati wa uzinduzi wa siku ya lishe, ambayo kitaifa imefanyika  jijini humo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku ya Lishe  uliofanyika Jiji Dodoma, ambapo amewataka  watumishi walio chini ya Ofisi yake kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto, ili kuhakikisha Watanzania wote wanafuata njia za sahihi zitakazowawezesha kuwa na lishe bora.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa...