TANZANIA KUANZA KUZALISHA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO UMRI CHINI YA MIAKA 5.

TANZANIA KUANZA KUZALISHA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO UMRI CHINI YA MIAKA 5.

NA MWANDISHI WETU

Tanzania iko mbioni kuachana na kuagiza vyakula vya nyogeza kwa Watoto kutoka nje ya nchi na matokeo yake vitaanza kuzalishwa hapa hapa nchini, mara baada ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na MUHAS, SUA na TBS kuja na mradi wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa ajili ya Watoto chini ya umri wa miaka mitano, ili kuhakikisha wanapata chakula kilichoboreshwa na kinachokidhi mahitaji yao.

 Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi huo Mkoani Morogoro Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Edward Mbanga kwa niaba ya Waziri wa Afya,   Ummy Mwalimu amesema hadi sasa hakuna hakuna uzalishaji wa kibiashara wa vyakula vya nyongeza hapa nchini na badala yake vimekuwa vikiagizwa kwa wazalishaji mbalimbali kutoka nje ya nchi.

 

Baadhi ya Viongezi  wa Taasisi zinazoshiriki kwenye mradi wa kutengeneza vyakula vya  nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya miakaa mitano, wakiangalia mojawapo ya mashine ambayo itatumika  katika uzalishaji wa vyakula hivyo, mara baada ya kutembelea eneo la kiwanda kitachotumika kuzalisha malighafi zitakazotumika kuandalia vyakula nyongeza, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Mbanga alisema Mradi huo ambao unafadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) utahusisha vyakula vya nyongeza vinavyopatikana nchini, ambavyo vimetajwa pia vitasaidia kuboresha matibabu ya Utampiamlo wa kadiri na vitatoa ajira kwa Watanzania watakaozalisha vyakula hivyo.

“Mradi huuu utakuwa msaada mkubwa kwa jamii kwani Utengenezaji wa vyakula vya nyongeza kwa ajili ya Watoto chini ya miaka mitan utasiadia kuzuia na kutibu utapiamlo wa kadiri nchini, na ni wazi vyakula vitakavyohusika ni vile ambavyo vinapatikana nchini”. Alisema Mbanga

 Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Chakula kutoka Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine Dk. Rashid   Juma akiwaonyesha wadau wa lishe (hawapo pichani) mfano wa unga utakaotengenezwa na kutumika   kuzalishia Chakula cha nyongeza, katika mradi wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa watoto   chini ya umri wa miaka mitano, ambao umezinduliwa Mkoani  na utatekelezwa na TFNC,MUHAS,   SUA NA TBS kupitia ufadhili wa WFP.

Awali akiwasilisha taarifa za namna mradi huo utakavyotekelezwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dk. Germana Leyna alisema   mradi huo utasaidia kuongeza upatikanaji rahisi wa chakula kilichotengenezwa ndani ya nchi kikiwa salama  kuweza kuwapatia Watoto lishe bora.

Dk. Leyna alisema pia vyakula hivyo vitaweza kupatikana kwa gharama nafuu na wameamua kufanya hivyo ili kuwezesha kila Mtanzania kuweza kumudu gharama zake na kuweza kumudu kukipata pindi atakapokihitaji.

 

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe akisikiliza maelezo ya namna vyakula vya nyongeza kwa Watoto chini ya Umri wa miaka mitano vitakavyoandaliwa, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Chakula katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine Dk. Rashid Juma wakati wa uzinduzi wa mradi  wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa ajili ya Watoto chini y miaka mitano.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe ambaye ni Washiriki pia kwenye mradi huo alisema suala la kuagiza vyakula vya nyongeza kutoka nje ya nchi kamwe halikubaliki hivyo kupitia mradi huu endapo utatekelezwa kama ulivyopangwa basi utasaidia kupunguza matatizo ya utampiamlo na udumavu kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Juliana Muiluri alisema wamejitoa kuhakikisha unafanikiwa, na endapo utafanyika kama ulivyokusudiwa basi utaweza kuitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa katik mapambano dhidi ya Utapiamlo na Udumavu.

 Mradi huu utaenda sambamba na kutafiti kuhusu ufanisi na kukubalika kwa vyakula hivyo hivyo kupitia mradi huu kutatengenezwa bidhaa za chakula kwa makundi mengine ya watu  kama vile wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

TUMIENI TAALUMA ZENU KUTATUA CHANGAMOTO ZA MASUALA YA CHAKULA NA LISHE KWENYE JAMII.