TAASISI YA CHAKULA NA LISHE YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI KUHUSU UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA

TAASISI YA CHAKULA NA LISHE YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI KUHUSU UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA

WANAHABARI nchini wametakiwa kutumia taaluma yao vizuri katika kuikumbusha jamii kuwa na uwajibu katika kuwawezesha wazazi kufanikisha unyonyeshaji ili kuboresha hali ya lishe ya watoto na kuendeleza nguvu kazi yenye tija kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.

Akizungumza wakati akifungua semina  ya siku moja ya wanahabari, Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Bi Sikitu Simon Kihinga, amesema kuwa vizuri kuyatumia vyema yale watakayojifunza ili kuendelea kutoa taarifa sahihi na kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya lishe


Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Bi Sikitu Simon Kihinga (kushoto) akiwafundisha waandishi wa habari dhana ya wiki ya unyonyeshaji  maziwa ya mama Duniani, semina iliyofanyika  katika ukumbi wa Taasiisi ya Chakula na Lishe Tanzania.

Bi. Kihinga amesema kuwa semina hiyo kwa wanahabari imelenga kuzungumzia maadhimisho wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani kwa mwaka huu, ambapo kuanzia Agosti 1 hadi 7 kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyengine duniania kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama.

Ameeleza kuwa maadhimisho hayo ni fursa ya pekee katika kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali na jamii ili kufikia malengo ya kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

"Mama anatakiwa kunyonyesha mtoto maziwa saa moja ya kwanza mara tu baada ya kujifungua pamoja na kuhakikisha mtoto anaendelea kunyonya mara kwa mara kadiri ya uhitaji wake bila kupangiwa ratiba" amesema Bi. Kihinga.

Waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti vya habari wakiwa katika semina ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani, iliyoandaliwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.

Amefafanua kuwa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani kwa mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu "Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira".

Ameeleza kuwa kauli hiyo imelenga kuwakumbusha mchango wa unyonyeshaji katika utunzaji wa mazingira ya dunia pamoja na kulinda afya.

"Jamii inatakiwa kuendelea na juhudi za kulinda, kuhimiza na kuendeleza na unyonyeshaji watoto maziwa ya mama kama njia mojawapo ya kupata matokeo chanya" amesema Bi. Kihinga.


Afisa Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Gelagister Gwarasa akiwasilisha mada kuhusu ulishaji wa watoto wachanga kabla ya kutimiza miezi sita wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyoendeshwa na TFNC katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kwa mwaka 2020 iliyobeba kauli mbiu inayosema “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira”

Bi. Kihinga amebainisha kuwa takwimu za hali ya ulishaji watoto nchini zinaonesha takribani asilimia 9 ya watoto wenye umri mdogo chini ya miaka miwili wananyonyeshwa na maziwa ya mama.

Amesema idadi ya watoto wanaoanzishwa vyakula vya nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 87, wakati idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo vya ubora kilishe ni asilimia 35.

Ameeleza kuwa ni muhimu kuendelea kukumbusha wajibu wa makundi mbalimbali ya wadau wa lishe kusaidia na kuondoa vikwazo vinavyochangia baadhi ya wanawake kushindwa kunyonyesha watoto wao kikamilifu.

Bi. Kihings amesema jamii inaitaji kutambua kuwa ili kuendelea usalama wa dunia na kizazi kijacho tunahitaji hatua za haraka ili kulea malenzi mazuri kwa mama kutokana unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni suluhisho majawapo ambalo linahitaji ushiriki mkubwa wa sekta mbalimbali ili kutatua changamoto.

Katika semina hiyo wanahabari wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo Afya ya lishe vijana balehe, Mama mjamzito na anayenyonyesha, ulishaji wa watoto wachanga kabla ya kutimiza meiezi sita, ulishaji wa watoto vyakula vya nyongeza (baada ya mienzi 6)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.