JAMII YAHIMIZWA KUSAIDIA MAJUKUMU YA KAZI MAMA ANAYENYONYESHA KUEPUSHA UTAPIAMLO KWA WATOTO
JAMII YAHIMIZWA KUSAIDIA MAJUKUMU YA KAZI MAMA ANAYENYONYESHA KUEPUSHA UTAPIAMLO KWA WATOTO
Na, TFNC Muheza
ULISHAJI usio sahihi unaochangiwa na mama kuelemewa na majukumu mengi ya kazi na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto ni sababu kubwa ya utapiamlo kwa watoto.
Hayo yamesema leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Muheza mkoani Tanga
"Ni dhahiri kuwa mchango wa mwanamke katika familia, ajira na uzalishaji kwa ujumla ni mkubwa hivyo ni muhimu kuwatia moyo na kuwasaidia wanawake ili waweze kufanya majukumu ya uzalishaji na utunzaji wa familia kwa ukamilifu.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya
Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama Duniani (hawapo Pichani) ambayo kwa mwaka huu
uzinduzi kitaifa umefanyika wilayani Muheza mkoani Tanga.Picha na Jackson Monela
Waziri Ummy amesema kuwa jamii ina wajibu wa kuwawezesha wazazi, hususani wanawake waweze kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akimkabidhi Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Tanga Burhan Yakubu kitini cha Lishe ya wanawake, Watoto na Vijana Balehe kwa ajili ya Vyombo vya Habari, kuashiria kuanza kutumika rasmi kwa kitini hicho, wakati wa Uzinduzi wa Wiki la Unyonyonyeshaji maziwa ya Mama Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika wilayani Muheza mkoani Tanga.
Aidha, amesema watoto
wanapotimiza miezi sita waanzishiwe vyakula vya nyongeza vyenye ubora kilishe
huku wakiendelea kunyonyeshwa hadi watakapotimiza umri wa miaka miwili.
Kwa upande wa takwimu za hali ya ulishaji watoto nchini Tanzania zinaonesha
kuwa takribani asilimia 97 ya watoto wenyeumri chini ya miaka miwili
wananyonyeshwa maziwa ya mama.
"Idadi ya watoto wanaoanzishiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa wakati
sahihi katika kipindi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 53 na
idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji
na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni
asilimia 58”, alisema Waziri Ummy.
"Vigezo hivyo ni
idadi sahihi ya milo anayopewa mtoto kwa siku kulingana na umri wake, na mlo
uwe na mchanganyiko wa vyakula kutoka kwenye makundi yasiyopungua manne ya
vyakula," amesisitiza.
Amesema Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kwa mwaka 2020 yamebebwa na
kauli mbiu inayosema “Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulizni wa mazingira"
Maoni
Chapisha Maoni