TAAASISI YA CHAKULA NA LISHE YAENDELEA KUWANOA WAANDISHI WA HABARI MIKOANI.

TAASISI YA CHAKULA NA LISHE YAENDELEA KUWANOA WAANDISHI WA HABARI MIKOANI.


Kaimu Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro Ester Clement Kawishe akiwasilisha mada kuhusu Hali ya Lishe pamoja na Umuhimu wa Siku 1000 za mwanzo za maisha ya mtoto wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari mkoani Morogoro iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Morogoro 21 Julai, 2020.


Wahariri wa vyombo vya habari mkoani Morogoro wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (hawapo pichani) wakati wa semina ya masuala ya chakula na lishe iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu  Kigurunyembe Morogoro.


Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya  Chakula na Lishe Tanzania Victoria Kariathi akiwasilisha mada kuhusu Mpango Jumuishi wa Utekelezaji wa Masuala ya Lishe (MNAP) 2016-20-21 wakati wa Semina ya Wahariri wa vyombo vya habari mkoa wa Morogoro ili kuwajengea uwezo wa namna ya kufuatilia habari  zinazohusiana na masuala ya Chakula na Lishe.

Afisa Mtafiti Msaidizi-Mawasiliano Hamza Mwangomale akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa wanahabari katika kufanikisha masuala ya Chakula na Lishe, wakati wa Semina ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika mkoani Morogoro.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.