WAZAZI NA WALEZI MSIOGOPE KUTUMIA VIRUTUBISHI MCHANGANYIKO KWENYE VYAKULA VYA WATOTO WENU.
WAZAZI NA WALEZI MSIOGOPE KUTUMIA VIRUTUBISHI MCHANGANYIKO KWENYE VYAKULA VYA WATOTO WENU.
Na, Jackson Monela, TFNC
Wazazi na Walezi katika Wilaya za Ikungi na Manyoni wametakiwa kuachana na imani potofu kuwa virutubisho mchanganyiko vina madhara kwa Watoto, na kuhofia kuvitumia, ilhali vimekuwa na msaada mkubwa katika kusaidia ukuaji mzuri wa mtoto na kusaidia katika kupambana na udumavu.
Wito huo umetolewa Mkoani Singida na Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi.Sikitu Kihinga, wakati wa mafunzo kwa watoa huduma za afya wa Halmashauri hizo, juu ya matumizi ya Virutubisho mchanganyiko ambavyo hutolewa kwa Watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23.
Sikitu amesema Virutubisho mchanganyiko vina umuhimu mkubwa sana kwa watoto kwani vinasaidia kupambana na tatizo la udumavu, ikizingatiwa katika jamii nyingi kumekuwa na changamoto baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kuandaa mlo unaokidhi mahitaji yote ya virutubishi vinavyohitajika kwa mtoto.
Halmshauri za Ikungi na Manyoni zipo kwenye utekelezaji wa mradi wa ugawaji virutubisho mchanganyiko kwa Watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23, ukiwa chini ya Ufadhili wa Shirika la Nutrition International na kusimamiwa na Shirika la World Vision, ambapo mpaka kufikia mwezi Machi 2020 katika halmashauri hizo mbili jumla ya Watoto 16416 wamefikiwa na huduma hiyo
Maoni
Chapisha Maoni