MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU

Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa wenyeviti pamoja na makatibu wa mashina ya chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya kisukuru jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI amesema mafunzo hayo yamefanyika kutokana na ombi la viongozi wa Kisukulu ambao waliomba taasisi ya MOI kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo na uwelewa viongozi hao ili wakawaelimishe wananchi wao.

"Tulipokea mamombi ya kuja kutoa elimu hapa, tukaona tuje kwani jukumu letu ni kutibu na kuelimisha pia hivyo tumewapa elimu kuhusu ugonjwa wa Corona lakini pia tumewatoa hofu kwani kumekua na uzushi mwingi kwenye miatandao ya kijamii" Alisema Dkt Boniface

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Moi Dkt: Respicious Boniface akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kisukuru, hatua mabazo zimechukuliwa na Taasisi hiyo katika kuhakikisha elimu ya Kukabiliana na ugonjwa wa Corona inatolewa na kuwafikia watu wananchi wote.

Pia Dkt Boniface amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya hapa nchini hivyo wananchi wasiwena na wasiwasi kwani vifaa vyote vipo na ni vya kisasa.

"Kuna uzushi mwingi kwenye mitandao kwamba hapa nchini kuna 'VENTILATOR' 2 habari hizo ni uzushi mtupu na nawaomba mzipuuze, pale Muhimbili ,MOI, JKCI tunazo zaidi ya 99 ambazo ni za kisasa kabisa ambazo zimenunuliwa na Serikali yetu tukufu" Alisema Dkt Boniface

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM kata ya Kisukulu Bw. Thomas Haule ameishukuru Serikali kwa jitihada kubwa za kupambana na ugonjwa wa Corona ambapo wananchi wamekua wakipata elimu na taarifa mbalimbali kuhusu ugonjwa huo.

" Nakushukuru sana Mkurugenzi kwa kuja kutupa elimu, tumeelimika na elimu hii itawanufaisha wananchi wetu wote wa kata hii ya kisukuru, Pia tunashukuru kwamba Serikali yetu ina watendaji ambao wanashuka mpaka chini, hatukutegemea kama Mkurugenzi kutoka MOI angefika hapa lakini leo amekuja na ametupa elimu" Alisema Bw. Haule

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kisukuru Minza Bakari akizungumza na viongozi wa chama hicho, umuhimu wa kufuatilia elimu na taarifa zinazotolewa na waatalamu wa Afya, katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona

Mkazi wa kata ya Kisukuru bwana Odacks Pembe ameshukuru kwa mafunzo waliyopata na kuahidi kuendelea kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

"Serikali kyupitia Wizara ya Afya imekua inafanya kazi nzuri na sisi wananchi tunashukuru sana kawani tunapata elimu, taarifa lakini pia huduma kwenye hospitali zetu ni nzuri, sisi wakazi wa Kisukuru tunaunga mkono jitihada za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli na tuko naye bega kwa bega" Alisema Bw. Pembe


Afisa Muuguzi  kutoka Kitengo cha Kuzuia Magonjwa ya Kuambukiza  cha Taasisi ya Mifupa Moi Georgina Chirwa akitoa maelekezo ya namna ya uvaaji wa  Barakoa kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kisukuru Tabata wilayani Ilala (hawapo pichani) wakati wa semina elekezi ya namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Pia Mkufunzi kutoka MOI Bi Georgina Chirwa amewaasa wananchi wa kisukuru kufuata maelekezo yote yanayotolewa na Wizara ya Afya ikiwemo kupuka mikusanyiko, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuvaa barakoa na endapo mtu ataona dalili kupiga simu no 199

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA LISHE YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI YATOLEWA

TFNC YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI.

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.