Jumapili, 11 Oktoba 2020

  TFNC YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mghumba (Mwenye skafu) akipokea maelezo ya makundi matano ya vyakula vilivyopo kwenye piramidi ya lishe kutoka kwa Afisa lishe mtafiti mwandamizi Mary Ngilisho wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania,mara baada ya naibu waziri kutembelea banda la Maonyesho la Taasisi hiyo, wakati wa uzinduzi wa wiki la maadhimisho ya siku ya chakula duniani, ambapo kwa hapa nchini kitaifa yanafanyika mkoani Njombe.

Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt: Elifatio Towo akitoa maelezo kwa naibu waziri wa Kilimo Omary Mghumba namna Taasisi hiyo inavyoshiriki katika uelimishaji na utafiti wa masuala ya Chakula na lishe, mara baada ya Naibu waziri kutembelea banda la Maonyesho la Taasisi ya Chakula na Lishe mara baada ya kuzindua Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Njombe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Francis Namaumbo (Mwenye kofia nyeupe) akisikiliza maelezo ya namna ya kutumia kaushio bora kwa ajili ya kukausha mbogamboga na matunda bila kuathiri virutubishi kutoka kwa    Mteknolojia wa mwandamizi wa Maabara Juvenary Mshumbusi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, mara baada ya mkurugenzi huyo kutembelea banda la Maonyesho la Taasisi hiyo katika  viwanja vya lunyanyo mkoani Njombe yanakofanyika maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.

 Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi Adeline Munuo akitoa elimu ya Masuala ya Chakula na Lishe kwa kutumia piramidi ya makundi matano ya chakula kwa baadhi ya wakazi wa Njombe, ambao wamepata fursa ya kutembelea banda la Maonyesho la Taasisi hiyo, katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani ambayo yanafanyika  kitafia mkoani Njombe na Kilele chake kinatarajiwa kuwa Oktoba 16.MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa...