SERIKALI INAHAKIKISHA WALENGWA WOTE WA CHANJO WANAFIKIWA KATIKA KIPINDI CHA CORONA
SERIKALI INAHAKIKISHA WALENGWA WOTE WA CHANJO WANAFIKIWA KATIKA KIPINDI CHA CORONA Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo imejipanga kuwafikia walengwa wote waliostahili kupata chanjo na kuhakikisha kiwango kinabaki vilevile kama ilivyotarajiwa. Hayo yamesemwa na Ofisa Mradi kutoka Mpango huo Lotalis Gadau wakati wa usimamizi elekezi wa kukagua utoaji huduma za chanjo katika Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Engender Health kupitia Merck Sharp& Dohme B.V (MSD). Gadau alisema kuwa katika kipindi hiki cha nchi kukabiliana na Ugonjwa wa Corona, Wizara imejipanga kuhakikisha watoa huduma wa afya wanaendelea kutoa huduma za chanjo kwa watoto wadogo pamoja na wasichana ambao walikua wapate chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi(HPV). “Kama Wizara tumejipanga vizuri kwa kuhakikisha chanjo zote zinakuwepo kwa wakati kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kuhakikisha watoto wote waliokuwa wanatara...