Machapisho

FEDHA ZA CRDB BANK MARATHON KUTUMIKIA KWENYE MATIBABU YA WATOTO WANAOTIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

Picha
FEDHA ZA CRDB BANK MARATHON KUTUMIKIA KWENYE  MATIBABU YA WATOTO WANAOTIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE Na, Mwandishi Wetu Dar es salaam. Benki ya CRDB imeandaa mbio za CRDB Bank Marathon kwa ajili ya kuchangisha fedha za matibabu ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezo wa kuchangia gharama za matibabu wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mbio hizo zitakazofanyika tarehe 16/08/2020 kuanzia saa 12 asubuhi jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa Habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema lengo la kuandaa mbio hizo ni kuleta tabasamu kwa watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na familia zao. Nsekela alisema licha ya kuandaa mbio hizo Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wenye matatizo ya moyo ambao w...