Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 28, 2020

TANZANIA KUANZA KUZALISHA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO UMRI CHINI YA MIAKA 5.

Picha
TANZANIA KUANZA KUZALISHA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO UMRI CHINI YA MIAKA 5. NA MWANDISHI WETU Tanzania iko mbioni kuachana na kuagiza vyakula vya nyogeza kwa Watoto kutoka nje ya nchi na matokeo yake vitaanza kuzalishwa hapa hapa nchini, mara baada ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na MUHAS, SUA na TBS kuja na mradi wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa ajili ya Watoto chini ya umri wa miaka mitano, ili kuhakikisha wanapata chakula kilichoboreshwa na kinachokidhi mahitaji yao.   Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi huo Mkoani Morogoro Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya   Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto   Edward Mbanga kwa niaba ya Waziri wa Afya,     Ummy Mwalimu amesema hadi sasa hakuna hakuna uzalishaji wa kibiashara wa vyakula vya nyongeza hapa nchini na badala yake vimekuwa vikiagizwa kwa wazalishaji mbalimbali kutoka nje ya nchi.   Baadhi ya Viongezi  wa Taasisi zinazoshiriki kwenye mradi wa kutengeneza vyakula