Alhamisi, 27 Agosti 2020

TFNC, KWA KUSHIRIKIANA NA MUHAS, SUA, TBS KWA KUPITIA UFADHILI WA WFP WAZINDUA MRADI WA KUTENGENEZA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5

TFNC, KWA KUSHIRIKIANA NA MUHAS, SUA, TBS KWA KUPITIA UFADHILI WA WFP WAZINDUA MRADI WA KUTENGENEZA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dk. Germana Leyna akiwasilisha taarifa ya mradi wa Kutengenezaa vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano kwa wadau wa lishe (Hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa mradi huo mkoani Morogoro, ambao utatekelezwa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na SUA, MUHAS na TBS kupitia ufadhili wa WFPBaadhi ya Viongezi  wa Taasisi zinazoshiriki kwenye mradi wa kutengeneza vyakula vya  nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya miakaa mitano, wakiangalia mojawapo ya mashine ambayo itatumika  katika uzalishaji wa vyakula hivyo, mara baada ya kutembelea eneo la kiwanda kitachotumika kuzalisha malighafi zitakazotumika kuandalia vyakula nyongeza, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.


Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe akisikiliza maelezo ya namna vyakula vya nyongeza kwa Watoto chini ya Umri wa miaka mitano vitakavyoandaliwa, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Chakula katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine Dk. Rashid Juma wakati wa uzinduzi wa mradi huo.


Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Edward Mbanga ambaye amemwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, akizungumza na wadau mbalimbali wa lishe (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutengeneza vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano uliofanyika mkoani  katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa...