Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 21, 2020

TFNC, KWA KUSHIRIKIANA NA MUHAS, SUA, TBS KWA KUPITIA UFADHILI WA WFP WAZINDUA MRADI WA KUTENGENEZA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5

Picha
TFNC, KWA KUSHIRIKIANA NA MUHAS, SUA, TBS KWA KUPITIA UFADHILI WA WFP WAZINDUA MRADI WA KUTENGENEZA VYAKULA VYA NYONGEZA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dk. Germana Leyna akiwasilisha taarifa ya mradi wa Kutengenezaa vyakula vya nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya Miaka mitano kwa wadau wa lishe (Hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa mradi huo mkoani Morogoro, ambao utatekelezwa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na SUA, MUHAS na TBS kupitia ufadhili wa WFP Baadhi ya Viongezi  wa Taasisi zinazoshiriki kwenye mradi wa kutengeneza vyakula vya  nyongeza kwa watoto wenye umri chini ya miakaa mitano, wakiangalia mojawapo ya mashine ambayo itatumika  katika uzalishaji wa vyakula hivyo, mara baada ya kutembelea eneo la kiwanda kitachotumika kuzalisha malighafi zitakazotumika kuandalia vyakula nyongeza, katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe akisikiliza

WAZIRI MHAGAMA AIASA JAMII KUTOPUUZA VYAKULA VYA ASILI

Picha
  WAZIRI MHAGAMA AIASA JAMII KUTOPUUZA VYAKULA VYA ASILI. NA.MWANDISHI WETU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameiasa jamii kuendelea kutumia vyakula vya asili ili kuwa na afya bora na kuondokana na magonjwa yatokanayo na lishe duni. Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Lishe unaoratibiwa na Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali chini ya ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe. Ziara hiyo iliyofanyika tarehe 20 Agosti, 2020 katika Halmashari ya Wilaya ya Songea pamoja na kutembelea zahanati ya Likarangilo iliyopo Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma katika kuadhimisha siku ya lishe kijijini hapo. Waziri Mhagama amesema kuwa, uwepo wa vyakula vya asili ni muhimu sana katika jamii zetu kwa kuzingatia vina virutubishi muhimu vya kuimarisha afya kwani hupatikana katika mazingira yanayozunguka na ni vyakula