Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 9, 2020

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.

Picha
  WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU. NA, TFNC DODOMA. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema atamwandikia barua Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kutoa pendekezo kuanzia Septemba Mosi Mwaka huu, Kila shule ya Msingi na Sekondari iwe na kibanda cha maziwa kwa ajili ya wanafunzi kupata lishe. Kauli hiyo aliitoa Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa siku ya Lishe Kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza maadhmisho ya siku hiyo yanafanyika nchini yakiratibiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau wengine wa Lishe nchini. Waziri Ummy alisema kuanzisha vibanda vya maziwa shuleni hasa shule za kutwa, kutasaidia wanafunzi kuboresha afya zao, lakini pia kutasaidia kupanua soko kwa bidhaa hiyo muhimu. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, pamoja na Naibu katibu Mkuu TAMISEMI (Afya)