Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 22, 2020

WANAHABARI MKOA WA MOROGORO WAOMBA KUJENGEWA UWEZO ZAIDI, KWENYE UANDISHI WA HABARI ZA LISHE

Picha
WANAHABARI MKOA WA MOROGORO WAOMBA KUJENGEWA UWEZO ZAIDI, KWENYE UANDISHI WA HABARI ZA LISH E. Na, Jackson Monela, Morogoro. Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) kimeiomba Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kuendelea kutoa mafunzo kwa waaandishi wa habari mkoani humo, ili kuzidi   kuwajengea uwezo wa kuripoti habari mbalimbali zinazohusu masuala ya chakula na lishe. Akizungumza wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wahariri na wanahabari wa mkoa wa Morogoro, namna ya kuhariri na kuandika habari zinazohusiana na Chakula na Lishe Mwenyekiti wa MOROPC, Nikson Mkilanya, amesema mkoa huo una zaidi ya waandishi wa habari 100, na 40 pekee ndio waliopatiwa mafunzo hayo, hivyo ameiomba Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kuendelea kutoa mafunzo hayo na kwa waandishi wengine mkoani humo. Mkilanya amesema kwa muda mrefu waandishi wa habari mkoa wa Morogoro walikuwa na kiu ya kupata elimu kuhusu masuala ya Chakula na Lishe, hivyo ameishukuruTaasisi ya Chakula na Lish