Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 27, 2020

HOSPITALI YA MIREMBE YABORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Picha
HOSPITALI YA MIREMBE YABORESHA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA. Na, Mwandishi wetu Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe imefanya mabadiliko katika utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje, ambapo muda wa kuanza kutoa matibabu ni saa moja asubuhi badala ya saa mbili asubuhi. Lengo la uongozi wa hospitali kufanya mabadiliko hayo ni kuboresha huduma za afya ili kuwezesha watu mbalimbali kupata huduma za matibabu mapema zaidi na kwa wakati. Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt. Paul Lawala amesema mabadiliko hayo yanahusu huduma zote za afya; ikiwamo huduma za afya ya akili pamoja na magonjwa ya mwili. Dkt. Isack Gesase wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe akimsikiliza mmoja wa wagonjwa waliofika kupatiwa Huduma ya matibabu hospitali hapo. Dkt. Lawala amesema tangu kuanza kwa utekelezaji wa mabadiliko hayo   kumekuwapo na matokeo chanya kwa kuwa watumishi wamefurahia kuanza kutoa huduma mapema, huku wagonjwa na ndugu wakifura