Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 12, 2020

MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU

Picha
MOI YATOA MAFUNZO YA CORONA KATA YA KISUKURU Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa wenyeviti pamoja na makatibu wa mashina ya chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya kisukuru jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI amesema mafunzo hayo yamefanyika kutokana na ombi la viongozi wa Kisukulu ambao waliomba taasisi ya MOI kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo na uwelewa viongozi hao ili wakawaelimishe wananchi wao. "Tulipokea mamombi ya kuja kutoa elimu hapa, tukaona tuje kwani jukumu letu ni kutibu na kuelimisha pia hivyo tumewapa elimu kuhusu ugonjwa wa Corona lakini pia tumewatoa hofu kwani kumekua na uzushi mwingi kwenye miatandao ya kijamii" Alisema Dkt Boniface Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Moi Dkt: Respicious Boniface akizungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kisukuru, hatua mabazo zimechukuliwa na Taasisi hiyo katika kuhakikisha elimu ya Kukabiliana na ugonjwa wa Corona inato