Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 7, 2020

WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU.

Picha
  WANAFUNZI WANYWE MAZIWA SHULENI-UMMY MWALIMU. NA, TFNC DODOMA. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema atamwandikia barua Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kutoa pendekezo kuanzia Septemba Mosi Mwaka huu, Kila shule ya Msingi na Sekondari iwe na kibanda cha maziwa kwa ajili ya wanafunzi kupata lishe. Kauli hiyo aliitoa Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa siku ya Lishe Kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza maadhmisho ya siku hiyo yanafanyika nchini yakiratibiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau wengine wa Lishe nchini. Waziri Ummy alisema kuanzisha vibanda vya maziwa shuleni hasa shule za kutwa, kutasaidia wanafunzi kuboresha afya zao, lakini pia kutasaidia kupanua soko kwa bidhaa hiyo muhimu. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, pamoja na Naibu katibu Mkuu TAMISEMI (Afya)

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA RASMI SIKU YA LISHE, SASA KUADHMISHWA KILA MWAKA KUANZIA NGAZI YA WILAYA HADI TAIFA.

Picha
  WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA RASMI SIKU YA LISHE, SASA KUADHIMISHWA KILA MWAKA KUANZIA NGAZI YA WILAYA HADI TAIFA. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akikata utepe kwenye  Piramidi ya Lishe, ambayo imebebea mfano wa Vyakula kutoka kwenye makundi matano ya Chakula, kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa  Siku ya Lishe, huku Naibu katibu mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt Doroth Gwajima (mwenye skafu) akishuhudua Uzinduzihuo  ambao umefanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (Kulia), na Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Doroth Gwajima (Kushoto) wakipokea maelezo ya vyakula vilivyopo kwenye Piramidi ya Lishe,kutoka kwa Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi Rose Msaki, mara baada ya kuzindua rasmi siku ya Lishe iliyofanyika  kitaifa Jijini Dodoma. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, akizungumza na Wananchi wa jiji la Dodoma na Wad