Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 23, 2020

SERIKALI YATOA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MAABARA YA TAIFA YA AFYA YA JAMII NA KUBAINI MAPUNGUFU MBALIMBALI

Picha
SERIKALI YATOA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MAABARA YA TAIFA YA AFYA YA JAMII NA KUBAINI MAPUNGUFU MBALIMBALI Na WAMJW – Dar es Salaam 23/05/2020  Serikali imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii iliyoko ofisi za Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadam (NIMR) jijini Dar es Salaam na kubaini mapungufu mbalimbali ya kiutendaji yaliyokuwepo katika maabara hiyo. Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametaja mapungufu yaliyobainishwa na kamati hiyo kuwa moja kati ya mashine za kupima sampuli za COVID-19 ilikuwa na hitilafu bila uongozi wa maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo. Taarifa hiyo pia imebaini kuwepo kwa upungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19.   Waziri Ummy amesema kamati hiyo pia